Joseph Panga Ashika Nafasi ya Tatu #BB10K

Mwanariadha wa Tanzania, Joseph Panga ashika nafasi ya tatu katika Mashindano ya Bolder Boulder Marathon 10K huko Marekani kwa kutumia dakika 29 na sekunde 3 (00:29:03) nyuma ya mkenya Bernard Ngeno aliyeshinda mashindano hayo kwa 00:28:29 akifuatiwa na delesa kutoka Ethiopia aliyeshika nafasi ya pili kwa 00:28:58.

Gabriel Geay ashika nafasi ya tano kwa muda wa 29:13 huku simbu akichukua nafasi ya kumi na nne kwa 30:16 katika mbio hizo za Bolder Boulder zilizofanyika tareje 27 Mei , 2019 nchini Marekani.

kwa upande wa wanawake , Magdalena Shauri ashika nafasi ya nane kwa kukimbia muda wa 34:05 huku Natalie Elisante akishika nafasi ya kumi na nne kwa kutumia muda wa 35:13

L-R, Fabiano Joseph Naasi , Joseph Panga and Emmanuel Giniki

Leave a reply