Mashindano ya Taifa ya Riadha 2019 Kufanyika Arusha.

Mashindano ya Taifa ya Riadha yatafanyika tarehe 5 na 6 Julai ,2019 katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Kwa udhamini wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na wachezaji 365 kutoka katika mikoa 31 ya Tanzania Bara na Visiwani wakimbatana na Viongozi 42 ili kusimamia mashindano hayo kwa mujibu wa sheria na kanuni za mashindano hayo kutoka Shirikisho la Vyama vya Kimataifa (IAAF).

Michezo itakayochezwa ni 14 kwa Wanaume na wanawake , ikiwemo ;

Mita 100 , 200 , 400 , 800 , 1500, 5000, 10000 pamoja na 4*100m na 4*400m.

Michezo mingine ni kama ;

Kurusha Mkuki , Kutupa Kisahani , Kutupa Tufe , Kuruka Chini na Miruko Mitatu.

Leave a reply