Mashindano ya Taifa Yameahirishwa kwa muda

Shirikisho la Riadha Tanzania inapenda kutangaza kwamba Mashindano ya Riadha ya Taifa yaliyopangwa kufanyika Arusha Julai 5 hadi 6 / 2019 yameahirishwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu.

Hata hivyo niwahakikishie wadau wote wa riadha nchini kwamba Mashindano ya Taifa yatafanyika baadae mwezi huu Arusha kwa tarehe itakayotangazwa wiki ijayo.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaotokana na ahirisho la Mashindano ya Taifa kwa tarehe iliyotangazwa awali.

Pia kwa niaba ya Shirikisho la Riadha Tanzania napenda kuujulisha umma wa watanzania kwamba tayari tumeshawasilisha majina ya wanariadha 15 BMT pamoja na taarifa zao kama tulivyoagizwa na BMT kuelekea Mashindano ya Afrika (All African Games) yatakayofanyika Rabat Morocco. Mawasilisho hayo yalifanyika tangu Juni 17 / 2019.

Pia RT tumeanza matayarisho ya timu ya Mashindano ya Dunia itakayofanyika kuanzia Septrmba 27 hadi Oktoba 6 / 2019 Doha Qatar, wanariadha watano waliofikia viwango stahiki wanatarajia kujinoa Iten Kenya (kambi ambayo inatumiwa na wanariadha nyota duniani).

Imetolewa na;

Wilhelm Gidabuday,
Katibu Mkuu / RT,
Julai 1, 2019.

Leave a reply